Kipaji au mambo unayopenda kuyafanya yanaweza kukutoa kimaisha

Pale unapokipenda kitu unachokifanya hakitaonekana kuwa kigumu hata kidogo.

Mawazo yako (2)

Jamii yetu wakati mwingine imekuwa ikitufundisha kuwa tutafute kazi kama sehemu ya kuanza kujipatia kipato ili kuzitimiza ndoto zetu. Lakini zipo njia zingine zinaweza kutusaidia kuja kupata kazi za ndoto zetu

Hebu fanya kufikiria kile kitu ambacho unapenda kukifanya kuliko kitu chochote duniani, na kifanyie utafiti katika jamii unayotoka ili uone kama unaweza kujitengenezea kipato kipitia kitu hicho.

Hii inaweza kuwa moja wapo ya njia zitakazokusaidia kupata kazi sahihi kwa ajili yako.

Kipindi mwandishi wa kitanzania aitwaye Halima alipokuwa bado binti mdogo, watu wengi walidhani angekuja kuwa daktari. Aliweza hata kwenda chuo kusomea ufamasia. Lakini moyoni mwake alikuwa na mipango mingine kabisaa. Halima alikuwa anapenda sana vitabu tokea alipokuwa mdogo. Hivyo aliamua kubadili mwelekeo toka kwenye masomo ya sayansi kwenda kwenye masomo ya uandishi mahiri na sasa hivi kazi yake ni Muandishi Huu ulikuwa uamuzi mgumu lakini alitambua kwamba kama angekuwa na kazi ya kitu anachokipenda basi ingempa furaha.

Hivyo, je kuna kitu unachokipenda ama unachofurahia kukifanya na ambacho kinaweza kukuingizia pesa? Labda unapenda kupika, unapenda michezo au sanaa? Je ndugu na marafiki zako huwa wanakuomba uwasaidie kufanya kazi zao za shule kwa sababu wewe ni mtaalamu zaidi kwenye somo hilo?

Basi kwa namna hiyo inawezekana ukawa umeshapata kazi maishani mwako.Unapofanya kazi hasa ya kile kitu unachokipenda itakufanya ujisikie poa kana kwamba haupo kazini.

Je unajiuliza unawezaje kuianza safari hii? Zifuatazo ni dondoo zitakazokusaidia kutimiza hili.

Fanya utafiti mdogo.

Zungumza na watu wanaofanya kazi, biashara unazopenda ili wakusaidie kuchagua njia sahihi kwa ajili yako. Kuna baadhi ya kazi, biashara au shughuli huwa zinahitaji kiwango maalumu cha elimu. Ila kwenye vitu vingine hili sio jambo la muhimu yaani unaweza ukatumia kipaji chako tu au ujuzi wako ili kujitengenezea kipato. Kwa mfano kazi za uDJ, MC au mpishi. Jaribu kufanya utafiti mara nyingi nyingi kadri unavyoweza kuhusu vitu unavyovipenda ili ujipange kuanza kupiga hatua

Unaweza kuanza hata leo.

Wakati mwingine huwa hatuhitaji vitu vingi ama pesa nyingi kuianza safari ya kazi au bishara za ndoto zetu.Je unaweza kuanza kujitolea hapo nyumbani kwenu, au katika jamii inayokuzunguka? Je unaweza kushirikiana na mtu ambaye tayari amekwishaanza kukifanya kitu kinachokuvutia ili upate ujuzi kutoka kwake? Kumbuka, kwa kupiga hatua ndogo ndogo zitakusaidia kujua vitu muhimu kuhusu hiyo kazi,pia itakusaidia kujua kama kweli upo tayari kukifanya kitu hicho katika maisha yako yote.

Jipe muda.

Jipe muda ili uweze kujua unapendelea kufanya nini hasa, na hata usijali kama bado haujui nini unatakiwa kufanya. Utumie muda huu kuangalia fursa mbali mbali na mara zote unaweza kubadili mawazo kama alivyofanya Halima.

Je kuna kitu ambacho unapenda kukifanya na unaona watu katika jamii unayoishi wanakifanya na kujitengenezea kipato? Tushirikishe maoni yako hapo chini.

Share your feedback

Mawazo yako

Kwan ukitaka kua na uwelewa mzur wa kupata pesa ufanye nini ili.ujipatie pesa kwa njia ya simu maan nishachoka kuhangaika na kufanya makaz yanguvu ambayo hayakupatii tija ya aina yoyote nifaye nini ili nipate pesa kiurahisi

Machi 20, 2022, 8:25 p.m

Nataka niwe na mchumba mwenye pesa zake Tena wa kiarabu nifanyeje na pia nataka nimroge mwanammke anipende nifanyeje

Machi 20, 2022, 8:25 p.m